Friday, February 13, 2015

LIGI kuu soka Tanzania bara inaendelea mwishoni mwa wiki hii kwa mechi kadhaa kupigwa viwanja mbalimbali nchini.

Kesho jumamosi (februari 14) Ndanda fc wataikaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.

Mtibwa Sugar wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha ‘mbwa mwizi’ cha mabao 5-2 walichopata dhidi ya mabingwa watetezi, Azam fc katika mechi ya ligi iliyopigwa jumatano, februari 11 mwaka huu.

Wagosi wa Kaya, Coastal Union watakuwa nyumbani CCM Mkwakwani Tanga kuchuana na Wagonga Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc.

Coastal wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya suluhu waliyopata dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita hapo hapo Mkwakwani, wakati Mbeya City fc walitoka sare ya bao 1-1 na JKT Ruvu uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mechi nyingine kesho itapigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga ambapo wenyeji Stand United watakabiliana na Maafande wa Ruvu Shootings kutokana Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Ligi hiyo itaendelea jumapili (februari 15) ambapo Polisi Morogoro wataikaribisha Simba kutoka Dar es salaam katika uwanja wa CCM Jamhuri, Morogoro.

Mechi iliyopita Simba walitoka suluhu na Coastal Union Mkwakwani, wakati Polisi Moro walifungana mabao 2-2 dhidi ya Azam fc uwanja wa Jamhuri.


Kagera sugar watakuwa na kibarua kizito dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video