Thursday, February 12, 2015

DSC_0210
Kiungo mahiri wa City, Steven Mazanda, anatarajia kurejea kikosini jumamosi hii kuivaa Coastal Union  kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara baada ya kuwa nje kwenye  mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa Chamanzi Complex kufuatia  kuwa na kadi tatu za njano.
Akizungumza  kuelekea mchezo huo wa jumamosi ulipangwa kupigwa jijini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani Mazanda alisema anafurahi kurejea tena kikosini kwa ajili ya kushirikiana na  wenzake kutafuta matokeo hasa baada ya kupata sare kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu.
“Kwanza nawashukuru wenzangu kwa kupambana na kupata sare mchezo uliopita, najua tulikuwa na hesabu za kupata pointi tatu lakini sare iliyotupa pointi moja siyo mbaya sana, nilikosa mchezo huo kwa sababu ya kadi za njano. ninayo furaha sasa kwa kuwa narejea kikosini kushirikina na wenzangu kusaka poiti 3 ambazo tukizipata tutakuwa tumesogea hatua nyingine kwenye msimamo wa ligi” alisema.
Katika hatua nyingine mshambuliaji Mwegane Yeya  naye atarejea kikosini jumamosi hii kuungana na safu ya nyota wawili Cosmas Fredy na Paul Nonga katika kusaka ushindi baada ya kuukosa mchezo uliopita kufuatia majeraha aliyopata  mazoezini  siku moja kabla ya kucheza na JKT Ruvu.
Yeya  amesema amefurahia kupona majereha na kurejea kikosini kuwavaa Coastal kwa sababu changamoto zilizopoa kwenye ligi hivi sasa hasa mzunguko huu wa pili zinahitaji kuwa sawa ili kuitumikia timu kwa nguvu zote .
“Changamoto za ligi hivi sasa ni kubwa kwa sababu huu ni mzunguko wa pili ambao hauhitaji kingine zaidi ya matokeo, nashukuru niko ‘fiti’ sasa kwa ajili ya kuitumikia timu, unahitaji kuwa vizuri ili uweze kupambana kwa sababu huu ndiyo wakati ambao ukilegea msimu ujao  utacheza daraja la kwanza” alisema Yeya na kuwafanya wachezaji wenzake kuangua kicheko..
DSC_0197
Yeya kushoto akiwa na David  Buruhani

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video