
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, wameunguruma katika
uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro baada ya kuitandika mabao 2-0 Polisi Moro
katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii.
Bao la kwanza la kikosi hicho cha Mserbia, Goran Kopunovic limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’
katika dakika nya 14’ ya kipindi cha kwanza.
Hadi dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika
Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Simba waliendelea kulisakama
lango la Polisi na katika dakika ya 63’ ya kipindi hicho, Elius Maguli
aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa kuandika bao la pili na la ushindi.
Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe pointi 20
baada ya kushuka dimbani mara 14 na sasa inazipumulia Yanga na Azam ambazo zipo
juu kwa pointi 5 zaidi.
Kujua nafasi ya Simba katika msimamo tunasubiria
matokeo ya Kagera Sugar na JKT Ruvu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Kabla ya mechi ya leo, Polisi Morogoro walikuwa
nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 19 kibindoni, wakifuatiwa na JKT Ruvu
wenye pointi 19.
Kama JKT Ruvu wamefungwa, basi Simba watapanda
mpaka nafasi ya tatu nah ii itakuwa faraja kubwa kwa Wana Msimbazi. Mtandao huu
unafuatilia kwa umakini matokeo ya huko na yakipatikana utajulishwa.
Azam wanaongoza katika msimamo wakijikusanyia
pointi 25 baada ya kushuka dimbani mara 13 sawa na Yanga wenye pointi 25 kwa
mechi 13 walizocheza, lakini wana Lambalamba wana wastani mzuri wa mabao ya
kufunga na kufungwa.

0 comments:
Post a Comment