Sunday, February 15, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa BDF XI FC, Letang Kgengwenyane amesema winga mzawa Mrisho Ngasa ndiye aliyekuwa mchezaji hatari zaidi wa Yanga SC katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini hapa jana.

Yanga SC iliutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana. Shukran kwa mabao mawili safi ya vichwa ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe katika dakika ya kwanza na 55.

Baada ya tu ya mechi hiyo, Kgengwenyane alisema Ngasa ndiye mchezaji hatari zaidi katika kikosi cha Yanga SC walichocheza nacho jana na kwamba ndiye aliyesababisha timu yake ilale kwa kipigo hicho ugenini.

"Yule namba 17 (Ngasa) ni hatari zaidi, anaujua sana mpira na ni msumbufu wakati wote wa mechi. Ndiye alisababisha mabao yote mawili," alisema kocha huyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video