Saturday, February 14, 2015

Msimu uliopita Simba walitoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro


WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wametamba kuvuna mzigo wa pointi tatu mbele ya wenyeji wao Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa kesho uwanja wa Jamhuri, Mji Kasoro Bahari, Morogoro.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amezungumza muda mfupi uliopita kuwa hali ya Morogoro ni shwari kabisa na wachezaji wote wapo katika morali ya ushindi.
"Tuko salama Morogoro, tumejiandaa vizuri sana. Hakika Polisi kesho hawachomoki, pointi tatu lazima watuachie". Amesema Nyasio.
Nyasio amesema baada ya suluhu ya Tanga, hawako tayari kupata matokeo kama hayo au kupoteza mechi licha ya ukweli Kwamba  Polisi ni timu nzuri na mechi ya mzunguko wa kwanza mwaka jana uwanja wa Taifa walilazimisha sare ya bao 1-1.
"Mwalimu Goran Kopunovic amefanya marekebisho katika kikosi chake, vijana sasa wameiva na kesho tunawaambia Wanasimba kuwa hatutafanya makosa ili kupanda katika msimamo wa ligi". Ameongeza Nyasio.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video