RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu
wa wilaya wapya 27 lakini katika idadi hiyo jina la Katibu Mkuu wa zamazi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Wilfred Mwakalebela limo ndani yake.
Mwakalebela amepata ulaji huo ambapo sasa
anakwenda kuiongoza wilaya ya Wanging’ombe iliyopo Njombe huku mwanahabari
Shabani Kissu akipelekwa Kondoa.
Akizungumza leo Mwakalebela ambaye
alikuwa katibu mkuu wa kwanza katika utawala wa Rais Leodgar Tenga amesema
ameishukuru serikali kwa kuona mchango wake kwamba anaweza kuisaidia nchi yake.
"Kwanza niishukuru serikali kupitia
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa kunioan bado nina mchango wa kuisaidia nchi
yangu lakini baada ya hilo nataka kufika katika kibarua changu hicho kujua
changamoto zinaziwakabili wananchi wa huko,"alisema Mwakalebela.
"Nikishafanya utambuzi huo sasa nitaanza
mikakati ya kuanza utatuzi kwa haraka nikisaidiana na wananchi wa huko, kikubwa
naomba ushirikiano kwa wakazi wenzangu wa Wang'ing'ombe."
0 comments:
Post a Comment