Wednesday, February 18, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Muda mfupi baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC kutamba kuendeleza ubabe wa kuipa vipigo timu ngumu kufungika nyumbani ya Ruvu Shooting Stars mkoani Pwani, maafande hao wameibuka na kusema wataitia adabu timu hiyo ya Chamazi jijini hapa katika mechi yao ya kesho.

Timu hizo zitakutana katika mechi ya kiporo ya raundi ya 15 ya Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani, uwanja ambao wenyeji wamepoteza mechi moja tu msimu huu.

Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting, ameuambia mtandao huu kwa simu muda mfupi uliopita kuwa wamejipanga kuwatia adabu Azam FC kama walivyofanya kwa Yanga SC na Mtibwa Sugar FC.

Timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ndiyo iliyokuwa ya kwanza kukifunga kikosi cha Mecky Mexime cha Mtibwa Sugar FC (2-1) kilichokuwa kimeshindikana katika michuano yote msimu huu.

"Ni mechi ngumu, lakini sisi ni wataalam wa kuwatia adabu walioshindikana. Kama ilivyokuwa kwa Mtibwa Sugar, tutafanya hivyo kwa Azam kesho, tutawatia adabu.

"Ni moja ya mechi zitakazotupa sifa kwa kuchukua pointi tatu toka Azam. Tumejiandaa na kujipanga kwa ajili ya ushindi," amesema Bwire.

Katika tambo zao Azam FC kupitia kwa msemaji wao, Jaffar Idd Maganga, wamesema kikosi chao kilichozitandika 5-2 Mtibwa Sugar FC na 2-0 El Merreikh FC ya Sudan katika mechi mbili zilizopita, kiko tayari kuendeleza ubabe dhidi ya timu hiyo ya jeshi inayomkosa beki wake wa kati kisiki George Michael aliyefungiwa mechi tatu kwa kumkaba koo straika Mrundi Amisi Tambwe wa Yanga SC.,

"Tunatambua Ruvu ni wagumu kufungika kwenye uwanja wao wa nyumbani, lakini tumejipanga vyema kwa ajili ya mechi zote msimu huu," amesema Mganga.

Azam FC inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog, ndiyo timu pekee ya nje ya mkoa wa Pwani iliyofanikiwa kuifunga Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini msimu uliopita, wakiichapa mabao 3-0.

Kikosi cha Mkenya Tom Olaba cha Ruvu Shooting Stars kimepoteza mechi moja tu kwenye uwanja huo msimu huu, kikilala 2-0 dhidi ya timu 'kibonde' msimu huu, Tanzania Prisons katika mechi ya kwanza ya msimu huu Septemba 20, mwaka jana.

Wanalambalamba wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 25 sawa na Yanga walioko nafasi ya pili, wakati Ruvu Shooting wako nafasi ya sita wakiwa na pointi 19 sawa na Mtibwa Sugar katika nafasi ya tano, Coastal Union (7), JKT Ruvu (8) na Polisi Moro (9).

Ruvu Shooting Stars iliyofungwa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo msimu huu Uwanja wa Azam jijini hapa Septemba 27, mwaka jana, itaingia uwanjani kesho jioni ikiwa na kumbukumbu ya kushinda 2-1 katika mechi zake mbili za nyumbani zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar FC na Stand United FC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video