
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeanika tarehe ya kufanyika kwa michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika Rwanda mwakani.
Kwa mujibu wa shirikisho hilo, michuano itaanza Januari 16 - Februari 7.
VIWANJA VINNE
Michuano hiyo itashirikisha timu 16 kutoka barani Afrika nha michezo itachezwa kwenye viwanja vinne ukiwamo wa Uwanja wa Umuganda uliopo Rubavu, Uwanja wa Huye, Uwanja wa Amahoro na Uwanja wa Kigali vilivypo jijini Kigali.
Hii ni michuano mikubwa zaidi kufanyika Rwanda ambao pia walikuwa wenyeji wa michuano ya 2009 ya vijana ya U20 barani Afrika na pia U17 barani 2011.
0 comments:
Post a Comment