
Wayne Rooney
LOUIS van Gaal amesisitiza kuwa Wayne Rooney ana furaha kucheza safu ya kiungo Manchester United, lakini atamrudisha tena safu ya ushambuliaji siku za usoni.
Kuna wasiwasi kuwa Rooney anaweza kuathirika kwa kucheza nafasi ya chini zaidi na uwezo wake wa kufunga magoli utashuka na tangu mwaka huu uanze hajapiga shuti lolote lililolenga lango.
Lakini Van Gaal ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa nahodha wake huyo anafurahia kazi yake kwenye timu hiyo na amekukuwa muhimu kutokana na timu kukosa uwiano na machaguo sahihi ya viungo.
"Ana furaha," Ameseama bosi wa United. "Vinginevyo angekuja kwamba na kuniambia hana furaha. Hajawahi kusema. Siku zote yuko karibu nami. Anahitaji kucheza vile ninavyotaka na hicho ndicho nakiona".

Louis van Gaal analipigia hesabu kombe la FA mwaka huu

0 comments:
Post a Comment