MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania , Azam fc
baada ya kufanikiwa kuibanjua Al Merreick ya Sudan mabao 2-0 katika mechi ya
kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika wametamba kurejesha nguvu zao kwenye
mitanange ya ligi kuu kabla ya kusafiri kwenda Sudan.
Mabao ya Azam fc jana yalifungwa na Didier
Kavumbagu na John Bocco kwa kila kipindi.
Azam fc itakabiliana na Ruvu Shootings katika
mechi ya kiporo ya VPL itayopigwa alhamisi ya wiki hii.
Baada ya mechi hiyo, Azam watashuka dimbani
jumapili ya wiki hii kuchuana na Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam
Complex.
Watakapomaliza mechi hizo mbili watasafiri kwenda
Sudan kucheza mechi ya marudiano ya klabu bingwa Africa.
Katika mechi hiyo, Azam fc wanahitaji sare ya 1-1
au kufungwa 1-0 kama wanataka kusonga mbele.
Al Merreick wao wanahitaji ushindi mkubwa wa mabao
3-0 ili kuwatoa mabingwa hao wa Tanzania bara.
Kwasasa Azam fc ndio vinara wa ligi kuu
wakijikusanyia pointi 25 kileleni sawa na Yanga katika nafasi ya pili, lakini
Wanalambalamba hao wanatamba kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam wamefunga magoli 22 na kufungwa magoli 12,
hivyo wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa ni 10.
Yanga wamefunga magoli 15 na kufungwa magoli 7 na
kuufanya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa kuwa 8.




0 comments:
Post a Comment