
Roy Hodgson (kulia) amemshauri Neville kujikita na ukocha kwa muda wote

Wachambuzi wa Sky Sports (kutoka kushoto kwenda kulia) Graeme Souness, Jamie Carragher, Thierry Henry, Jamie Redknapp na Neville.
ROY Hodgson amemshauri msaidizi wake Gary Neville kuachana na uchambuzi wa soka kwenye TV na kujikita na kazi ya ukocha wakati huu mzee huyo akitafakari maamuzi yake ya kuendelea na ukocha mwaka 2016 au la!.
Neville ambaye anatajwa kumrithi Hodgson kama ataachana na kazi ya kuifundisha England baada ya michuano ya kombe la mataifa Ulaya mwaka 2016, alisema atafanya maamuzi mwakani kama ataendelea na utangazaji au kujikita na mpira, akitambua kuwa hawezi kutumikia kazi zote mbili kwa wakati mmoja.
Kama Hodgson ataamua kustaafu mwaka 2016 huku timu imefanikiwa, Neville ndiye atakuwa mrithi wake, lakini Hodgson anaamini kuwa muda ukifika, itabidi msaidizi wake huyo aachane na masuala ya vyombo vya habari.

0 comments:
Post a Comment