HAKIKA Simba walimnunia golikipa wa Stand United
John Mwenda kwa kuchangia kuwanyima ushindi jana Kambarage, Mnyama akivutwa
sharubu 1-0 katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na mtandao huu, Mwenda amesema umahiri
wake langoni unachangiwa na nidhamu ya mazoezi, umakini na kuwasoma
washambuliaji pinzani.
“Nazingatia sana mazoezi ya makocha wangu, mpira
hauna uchawi, niliweza kuokoa michomo hatari ya Simba kwasababu ninajituma
katika mazoezi”. Alisema kipa huyo akiwa kwenye pozi la aina yake la picha.
0 comments:
Post a Comment