KOCHA mkuu wa Simba SC, Mserbia, Goran Kopunovic,
jana hakuwa na mpango wa kuongea na waandishi wa habari baada kuchapwa bao 1-0
dhidi ya Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage,Shinyanga.
Hata hivyo wanahabari ‘mapaparazi’ hawashindwi kitu,
walimfuata na kumuweke vinasa sauti wakimtaka atie neno kwa ajili ya
wasikilizaji, wasomaji na watazamaji.
Akiwa hana hamu ya kuongea, Kopunovic alisema : “Ligi
ni ngumu, mechi ilikuwa kama fainali. Nimeona timu zinaikamia Simba, lakini
bado tutaendelea kujiandaa kwa kila mechi iliyombele yetu”.
“Tunafanya kazi kwa juhudi, kwa asilimia 100
niifundisha timu, matokeo yamekuwa ya kupanda na kushuka, kwa pamoja tutapata
mafanikio”
Machi 8 mwaka huu, Kopunovic atawavaa Yanga katika
mechi ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Huu utakuwa mtihani mkubwa kwa Mserbia huyo kwani mechi
zinazowakutanisha watani wa jadi Tanzania (Simba na Yanga) huwa zinachangia
kufukuzwa kwa makocha.
0 comments:
Post a Comment