Kapombe (kushoto) siku walipocheza na Simba
MCHEZAJI kiraka wa Azam fc, Shomari Salum Kapombe
amesema matokeo mabaya wanayopata Prisons ndio chanzo cha kuwakazia jana usiku
katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika kwa suluhu uwanja wa Azam
Complex.
“Prisons walifungwa mechi iliyopita na Yanga, leo
wamekuja na nguvu. Wameonesha kiwango kizuri na nidhamu ya mchezo. Wamejilinda
vizuri na kucheza mpira”.
“Tumejitahidi kufika mara nyingi golini kwao,
lakini kipa wao (Mohammed Yusuph) amekuwa imara”.
Kwa matokeo ya jana, Azam fc wanaendelea kushika
nafasi ya pili kwa pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 15, wakati Yanga
wanaongoza msimamo kwa pointi 31 baada ya kucheza mechi 15.
Kapombe amesema baada ya mechi hiyo, sasa
wanaelekea macho yao katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa barani
Afrika dhidi ya Al Merreick.
Mechi ya kwanza Azam walishinda 2-0 na mechi ya marudiano
itayopigwa mwishoni mwa wiki hii, matajiri wa Dar wanahitaji ushindi au
kufungwa magoli yasiyozidi mawili.
0 comments:
Post a Comment