MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Azam fc wamelazimisha suluhu (0-0) ugenini dhidi ya wenyeji Ruvu Shootings katika
mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa
Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Kwa dakika zote 90’ timu zote zilicheza soka la
uangalifu na kuzuia mianya ya kufungwa goli.
Ruvu Shootings walikuwa makini zaidi katika mechi ya
leo kuhakikisha hawagawi pointi tatu kama walivyofanya msimu uliopita
walipofungwa 3-0 na Azam fc katika uwanja wao.
Awali walitamba kuwazuia Azam fc kupata pointi
tatu kwa kuwafunga na katika mechi leo, lakini wamefanikiwa kufanya kupata
pointi moja.
Dakika za lala salama timu zote zilitengeneza
mipango ya kufunga magoli, lakini makipa wa timu zote walisimama imara.
Dakika ya 80’ ya mchezo, John Bocco aliachia shuti
kali, lakini mlinda mlango wa Shootings, Rashid Abdallah alipangua na mabeki
wakaondosha mpira eneo lao la hatari.
Dakika ya 82’ Michael Aidan almanusura awafungie
Shootings kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake likaokolewa na kipa Aishi
Manula na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90’ zinamalizika, Ruvu Shootings 0 Azam
fc 0.
Azam walifanikiwa kupiga mashuti 7 yaliyolenga
lango dhidi ya 6 ya Ruvu Shootings .
Pia Azam walimilika mpira kwa asilimia 52 kwa 48
za Ruvu Shootings.
Kwa matokeo hayo, Azam FC wamefikisha pointi 26
kileleni wakisubiri matokeo ya Mbeya ambapo Yanga wanaongoza mabao 2-0 mpaka
sasa.
Azam fc wamebaki na magoli yao 22 ya kufunga na 12
ya kufungwa, hivyo wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa ni 10.
Ruvu Shootings wao wamefikisha pointi 20 na kupanda mpaka nafasi ya 5 kutoka ya 9.
Nafasi ya nne inaendelea kushikiliwa na Simba
wenye pointi 21.

0 comments:
Post a Comment