
Sergio Aguero (kulia) na nyota wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) wanajulikana kuwa marafiki wa karibu
SERGIO Aguero na mpenzi wake Karina Tejeda walifurahia wikiendi mjini Barcelona na alikutana na Muargentina mwenzake Lionel Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo.
Mshambuliaji huyu wa Manchester City, Aguero amekuwa akihusishwa kujiunga na Barcelona amesafiri kwa ndege binafsi kurudi England ili kuungana na wenzake katika mazoezi ya mabingwa wa ligi kuu England leo jumatatu.
Vyombo vya habari vya Barcelona vinashawishika kuamini kuwa Messi anamtaka Aguero kuungana na miamba hiyo ya Hispania mapema wakimaliza adhabu yao ya kufungiwa usajili mwaka 2016.

Aguero aliposti picha kwenye akaunti yake ya Twita juni 24 akimtakia sherehe njema ya kuzaliwa Lionel Messi.

Mpenzi wa Aguero, Karina Tejeda aliposti picha hii siku ya wapendanao 'Valentine's Day '

0 comments:
Post a Comment