Thursday, February 12, 2015

DSC_0229
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kukata mbuga jumamosi hii kwa michezo kadhaa ya mzunguko wa pili, Kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Mbeya City fc  itashuka  uwanjani hapo kucheza dakika 90 kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu na pia kulipa kisasi kwa wagosi hao kufuatia kupoteza mchezo kama huo msimu uliopita.
Akizungumza mapema leo jijini hapa, kocha wa City, Juma Mwambusi, amesema amewaandaa  vizuri  nyota wake kuhakikisha  wanashinda  mchezo huo wa jumamosi ili kujiongezea pointi 3 muhimu ambazo zitaiwezesha City kusogea nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi na pia kulipa kisasi kwa Coastal Union ambayo  ilikuwa timu ya pili kutibua mipango ya City kutwaa ubingwa msimu uliopita baada kushinda bao 2-0  kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
“Tunafahamu Coastal walitufunga  msimu uliopita, mara hii tunarudi Mkwakwani tukiwa na lengo moja la kushinda na kuondoka na pointi zote 3, nimeiandaa vizuri timu yangu ili tufanikiwe hilo, kama ujuavyo matokeo kwenye mchezo mmoja yanakusogeza kwenye nafasi nyingine katika msimamo wa ligi hicho ni kitu pekee ambacho tunakitizama sana , nashukuru mungu vijana wote wako kwenye hali nzuri kwa maana kuwa hatuna majeruhi kikosini imani yangu kubwa kuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutaibuka na ushindi” alisema.
DSC_0302Kocha Mwambusi (katikati) akielekeza jambo

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video