Thursday, February 19, 2015

KOCHA mkuu wa Azam fc, Joseph Marius Omog imemuanzisha golini mlinda mlango imara, Aishi Salum Manula katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shootings inayopigwa jioni ya leo uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Manula alifanya kazi kubwa Azam ikiifunga mabao 2-0 Al Merreick ya Sudan katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika iliyopigwa mwishoni mwa wiki uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Beki wa kulia ameendelea kuwa Shomari Kapombe,  kushoto Erasto Edward Nyoni na mabeki wa kati ni Said Moradi na Pascal Wawa.
Omog amelazimika kufanya mabadiliko ya nafasi ya mabeki wa kati kwa kumtoa Aggrey Morris aliyecheza dhidi ya Merreikc kwasababu anatumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi 3 kutokana na kosa la kumpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Anord Okwi.
Kiungo wa ulinzi ameanza Mudathir Yahya 'Scholes' ambaye hakucheza mechi ya Al Merreick kwasababu ya kukosa uzoefu wa michuano mikubwa barani Africa.
Himid Mao Mkami ameanza wingi ya kulia, wakati kiungo mchezeshaji ameanza Frank Domayo 'Chumvi'.
Mshambuliaji mwandamizi, John Raphael Bocco 'Adebayor' ameanza nafasi ya mshambuliaji wa kati, huku Salum Abubakar 'Sure Boy' akicheza nyuma yake.
Mechi ya Al Merreick alitokea benchi akichukua nafasi ya Kavumbagu ambaye leo ameanzia benchi.
Bocco na Kavumbagu walifunga goli moja moja na kuipa ushindi Azam fc.
Winga wa kulia ameanza Kipre Herman Tchetche.
Wachezaji wa akiba ni Mwadini Ali, Gadiel Michael, David Mwandika, Didier Kavumbagu, Amri Kiemba, Khamis Mcha 'Vialli' na Kelvin Friday.

KIKOSI CHA LEO  AZAM FC HIKI HAPA
1. AISHI MANULA 
2. SHOMARI KAPOMBE 
3. ERASTO NYONI 
4. SAID MORAD 
5. PASCAL WAWA
6. MUDATHIR YAHYA
7. HIMIDI MAO
8. FRANK DOMAYO
9. JOHN BOCCO
10. SALUM ABUBAKAR
11 KIPRE TCHETCHE
AKIBA
1. MWADINI ALI
2. GADIEL MICHAEL
3. DAVID MWANTIKA
4. DIDIER KAVUMBAGU
5. AMRI KIEMBA
6. KHAMISI MCHA
7. KELVIN FRIDAY

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video