KOCHA mkuu wa Simba , Goran Kopunovic katika
mazoezi yake anatumia muda mwingi kuwafundisha wachezaji wake mambo makubwa
matatu ambayo ni kumiliki mpira, kukaba na kushambulia kwa mpira ya krosi.
Katika mazoezi yake jana uwanja wa Amaan,
Kopunovic muda mwingi aliwaacha wachezaji wake wacheze soka huku akionesha kwa
vitendo namna ya kupiga pasi sahihi, kufungua nafasi na kuachia mpira.
Pia aliwaelekezea namna ya kupiga mipira ya krosi,
mashuti na mikwaju ya penalti.
Kocha huyo dhahiri anapenda kumiliki sana mpira na
maandalizi yake yamejikita katika hilo.
Mazoezi ya jana yalikuwa maalumu kwa mechi ya leo usiku ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi
dhidi ya Polisi Zanzibar.
Kopunovic anahofia kwamba timu yake inaweza kufika
hatua ya penalti na ndio maana aliwafundisha wachezaji wake namna ya kuwafunga
magolikipa kiufundi.


0 comments:
Post a Comment