Ivo Mapunda akifanya mazoezi jana uwanja wa Amaan
GOLIKIPA mkongwe wa Simba SC, Ivo Philip Mapunda
amerejea kambani kufuatia kutokuwepo kwa siku tisa akikamilisha 40 za mama yake
mzazi aliyefariki dunia mwishoni mwa mwezi novemba.
Mapunda alitua jana mjini Zanzibar na kuungana na
wenzake katika mazoezi ya jioni yaliyofanyika uwanja wa Amaan kujiandaa na
mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi itakayopigwa usiku wa leo baina ya
Simba na Polisi Zanzibar.
Akizungumza na mtandao huu, kipa huyo wa zamani wa
Tanzania Prisons, Yanga, Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia alisema
kwasasa hayuko fiti kucheza mechi.
“Nimeingia leo (jana) hapa hapa Zanzibar na kuanza
mazoezi jioni hii. Sikuwepo kwa muda siku tisa. Niliondoka tarehe moja”. Alisema
Ivo. “Hapa mpaka niamshe amshe viungo, si unajua vililala kwa muda”.
Ivo ndiye aliyesimama langoni Simba ikichapwa bao
1-0 na Kagera Sugar, desemba 26 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam na
kuamsha hasira za mashabiki wa Simba.
Goli hilo lilifungwa na Atupele Green katika
dakika ya 21 akimalizia mpira wa kurushwa ambapo Mapunda alishindwa kuucheza.
Kipigo hicho kilimfukuzisha kazi kocha Patrick
Phiri na mikoba yake kuchukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic.


0 comments:
Post a Comment