Saturday, September 6, 2014

Hatima ya Mshambuliaji wa Simba sc, Mganda Emmanuel Okwi (katikati) ni kesho

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam


UONGOZI wa Simba sc umepokea kwa furaha ushindi wa mabao 3-0 walioupata mbele ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa jioni ya leo uwanja waTaifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Paul Kiongera, aliyetia kambani mawili na moja likizamishwa nyavuni na Ramadhan Singano ‘Messi’.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo alisema wamefurahishwa na ushindi, lakini kubwa zaidi ni namna timu ilivyocheza kwa kiwango cha juu.

“Kwa kweli tumepokea kwa furaha matokeo, lakini kubwa sio ushindi peke yake bali ni jinsi gani timu imeweza kutandaza mpira chini”.

“Timu imecheza mpira maridhawa, imecheza kitimu  na kuwa na mipango ya kushambulia na kutumia nafasi”. Alisema Kaburu.

“Kimsingi mambo haya kama uongozi yametufurahisha na tunaamini timu itazidi kuimarika muda hadi muda kuelekea ligi kuu soka Tanzania bara”.

Pia Kaburu alimzungumzia mshambuliaji wao Emmanuel Okwi ambapo alisema nyota huyo alicheza mpira mzuri na kusababisha magoli yaliyofungwa leo hii.

Kaburu aliongeza kuwa Simba haina tatizo na Yanga bali Okwi ana matatizo na Yanga , lakini hapo kesho jibu litapatikana kutoka kwa kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania.

Kiongozi huyo alisema Simba imepeleka majina matano ya wachezaji wa Kigeni akiwemo Okwi, lakini beki wao Mkenya Donald Mosoti hajajumuishwa licha ya kuwa na mkataba.

Kaburu alisema wanafanya taratibu za kumalizana na Mosoti na wakati wowote ataondoka nchini.

Na kama Okwi hatapitishwa, Kaburu alisema Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kutandaza soka.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video