
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MLINDA mlango mkongwe nchini, Juma Kaseja
anatarajia kusimama katika milingoti mitatu,
Yanga ikiikabili Big Bullets FC (zamani Bata Bullets) ya Malawi ndani ya
dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Hali hiyo inatokana na mlinda mlango namba moja wa
klabu hiyo, Deogratius Munish kuwa katika majukumu ya timu ya Taifa, Taifa
Stars , itakayocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya
FIFA dhidi Burundu kesho mjini Bujumbura.
Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’
amesema Yanga ina makipa watatu wenye kiwango cha kuu na yeyote yule anaweza
kufanya kazi nzuri uwanjani.
“Siri yetu sisi ni kwamba makipa wetu watatu, Juma
Kaseja, Ally Mustapha na Deogratius Munish ‘Dida’ wanafanya mazoezi katika
kiwango cha juu na ni makipa bora”.
“Mifano iko hai, katika mchezo iliofanyika Pemba
tulishinda bao 1-0 na kule Ungaji kila tulipocheza tulishinda 2-0. Matokeo haya
yanaonesha makipa na safu ya ulinzi wako
sawasawa,”
“Makipa wangu wote wako katika kiwango cha
kufanana.Hatuna matatizo katika mchezo wa kesho kwasababu makipa wanafanana.
Hata kule Zanzibar mwalimu Maximo alikuwa anatoa timu nzima, anaanzisha
golikipa na timu yake nyingine”.
Katika kikosi cha pili cha Yanga mara zote langoni
anasimama Kaseja, hivyo ni dalili tosha kuwa kesho ndiye atakayeanza kama
hatakuwa na tatizo lolote.
Tayari Big Bullets wameshatua Dar es salaam na
maandalizi kwa ajili ya mechi yamekamilika.
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema
wachezaji wote wapo katika morali ya juu na mechi hiyo inatarajia kuanza majira
ya saa 10:00 jioni kwa mujibu wa waandaaji wa mechi DRFA.
0 comments:
Post a Comment