Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Polisi Morogoro katika uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni siku maalumu ya timu hiyo "Coastal Union Day
Siku hiyo pia itakuwa maalumu kwa ajili ya utambulisho kwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotazamiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa
El Siagi amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.
Amesema siku ya kesho itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu,El Siagi amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
0 comments:
Post a Comment