Imechapishwa Agosti 6, 2014, saa 8:04 mchana
MSHAMBULIAJI wa PSG , Zlatan Ibrahimovic anataka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Juventus, kwa mujibu wa mahojiano na kocha kocha wake wa zamani wa Malmo, Stefan Hansson kwenye gazeti la Tuttosport.
Nyota huyo amefurahia kucheza soka lake kwa mafanikio makubwa katika nchi za Italia na Hispania na sasa mshambulaiji huyo mwenye maiaka 32 anataka kurudi Seria A kwa miamba ya Italia.
Ibrahimovic alicheza miaka miwili Turin kuanzia mwaka 2004 hadi 2006.


Naitaka Juve: Ukurasa wa mbele wa gazeti laTuttosport ulikuwa na kichwa cha habari kilichoonesha kuwa Ibrahimovic anataka kurudi Juve majira haya ya kiangazi.
Hata hivyo, Hansson ameweka wazi kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alimwambia katika mazungumzo ya Skype na kumueleza kuwa anahitaji kujiunga na Juvetus.
Alisema: 'Niliongea na Ibra kwasababu bado tuna mahusiano mazuri tangu nilipomfundisha akiwa mtoto huko Malmo.

Ibra enzi zake Juventus
0 comments:
Post a Comment