
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu
akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto
kwake ni Kocha Mkuu Marcio Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Imechapishwa Agosti 6, 2014, saa 8:17 mchana
UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na
kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza
sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu
Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa
kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo
kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
"Baada
ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya
wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano
hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho
tulitimiza" alisema Beno.
Lakini
katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA
imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu
ya Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni za
CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima
wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo
orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha
Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki
michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua
dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi
ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na
jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji
watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua
na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini
walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa
kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio
Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo
ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho
kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti
ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza
wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya
kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu
uliopita.
b)
Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa
Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti,
takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c)
Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi
wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo
wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana
hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d)
Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho
wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni
za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza
mpira kwa ligi ya ndani.
e) Katika
wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6
wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi
ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f)
Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya
kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika
ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yanga
tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha
kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa
wachezaji wake.
0 comments:
Post a Comment