
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 6:22 mchana
WAYNE Rooney ameifurahia nafasi yake chini ya
kocha mpya Louis van Gaal na anaamini kuna dalili za kufanya vizuri msimu ujao
zipo wazi.
Msimu uliopita, nyota huyo mwenye miaka 28
alifunga mabao 17 na kusaidia mengine 12 chini ya kocha David Moyes, lakini Man
United iliishia nafasi ya 7 katika msimamo na kukosa michuano ya Ulaya.
Rooney anaamini timu yao imerudi katika makali yake
chini ya Mholanzi na anasema anafurahi sana kucheza katika mfumo mpya wa 3-5-2
ambao umemfanya afunge mabao manne katika mechi tatu za maandalizi ya msimu.
“Mfumo umekuwa mzuri,” mshambuliaji huyo
aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa Michigani. “Kiukweli kocha
amekuja na tumekuwa tukifanya mazoezi katika mifumo tofauti, lakini ni mizuri
mno, hata katika umri wangu najifunza vitu vipya na nitakuwa mzuri sana.
“Tunatakiwa kujiboresha zaidi na wiki chache
zijazo, nina uhakika tutaweza. Naamini matokeo mazuri yatazidi kuja kuanzia
jumamosi (leo)”.
Manchester United itacheza na Real Madrid leo
katika mechi ya michuano ya kimataifa ya kirafiki na wakishindwa watatinga
fainali. Licha ya kuwa michezo ya kirafiki, Rooney anatarajia kufunga mabao na
kumaliza kama vinara wa kundi lao.
“Inaweza kuwa nzuri sana kucheza na mahasimu wetu
Manchester City katika mchezo wa fainali, lakini kwanza tuna mchezo na Real
Madrid (leo) na ni muhimu kwetu kushinda,” Nyota huyo wa England aliongeza.
0 comments:
Post a Comment