
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 6:06 mchana
ASERNE Wenger anaamini Alexis Sanchez aliathirika
kama anavyoathirika Neymar wakati akiwa Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel
Messi.
Asernal ilitumia Euro milioni 40 kumsajili nyota
huyo wa kimataifa wa Chile majira haya ya kiangazi na leo hii anatarajia
kucheza mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Licha ya kucheza kama winga akiwa Barca, Alexis
atachezeshwa kama mshambuliaji Emirates na Wenger anaamini atang`ara zaidi
katika nafasi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ‘mchawi’ wake Messi.
“Kwa mara ya kwanza alitinga katika rada zangu
alipokuwa Udinese na baadaye Barcelona”. Alisema Mfaransa huyo alipozungumza na
The Dail Mirror.
“Ni mshambuliaji. Ni mmaliziaji mzuri ambaye
alikuwa na kiwango kizuri Italia. Nilimuona pale na alikuwa amesimama vizuri.
Lakini mambo yalikuwa magumu alipoenda Barcelona kama ilivyo kwa Neymar sahizi”.
“Unapomuona Neymar wa Brazil na Neymar wa
Barcelona sio mtu mmoja. Naamini kuwa Alexis anaweza kucheza kushoto, kulia na
mbele na ndio maana nilimfuata”.
0 comments:
Post a Comment