Mwakilishi
wa wanachama wa Coastal Union,Salim Al Mazrui akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari jana.
Na Mwandishi Wetu, Tanga
Imechapishwa Agosti 8, 2014, saa 7:55 mchana
MKUTANO
mkuu wa dharura wa wanachama kujadili kuhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal
Union, Hemed Aurora kujiuzulu unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii kwenye
ukumbi wa Makao makuu ya Klabu ya Coastal Union barabara ya 11 jijini Tanga.
Mkutano huo
unatarajiwa kuanza saa nne asubuhi utakaohusisha wanachama hai ambao wamelipia
kadi zao na hawadaiwi madeni yoyote.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mwakilishi wa Wanachama wa Coastal Union, Salim
Al-Mazrui alisema maandalizi ya kuelekea mkutano huo yamekamilika kwa asilimia
kubwa na utakuwa na agenda mbili muhimu zitakazojadiliwa.
Al Mazrui
alisema agenda ya kwanza itakuwa ni kujadili uvumi uliojitokeza wa kujadili
kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Hemed Hilal
Aurora.
Alisema agenda
ya pili itakuwa ni kujadili utendaji wa Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mguto ndani ya klabu hiyo hasa kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania
bara na kutoa maamuzi.
Mwakilishi
huyo aliwataka wanachama wa Coastal Union waliokuwa hai kuhakikisha
wanajitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wenye lango pia la kuangalia namna ya
kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kuu.
Kwa upande
wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alithibitisha kupokea taarifa
ya mkutano huo na hivyo utafanyika siku ya Jumapili kutokana na wanachama hao
kufuata taratibu zote.


0 comments:
Post a Comment