
Mchezaji kutoka
Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu na mashabiki
katika mchezo wa ligi nchini Algeria.
Ebosse, 24,
alithibitishwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi
Ouzou, mashariki mwa mji mkuu, Algiers.
Mshambuliaji huyo
wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa amefunga goli moja katika mchezo huo waliopoteza kwa
2-1, dhidi ya USM Alger aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika,
wakati wachezaji wakiwa wanatoka uwanjani.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka
uchunguzi kufanyika mara moja.
Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa
nacho, lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa
na kufungwa na walikuwa wakirusha mawe.
Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema
:"alikufa kutokana na jeraha la kichwani" baada ya kurushiwa kitu
mwisho wa mchezo.
Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika,
Issa Hayatou ametoa taarifa inayolaani tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment