Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 7, 2014, saa 1:19 jioni
MSAFARA wa wachezaji 20 na viongozi wa Azam fc umekwea pipa jioni ya leo kwenda
mjini Kigali nchini Rwanda kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki
na kati maarufu kwa jina la Kombe la Kagame.
Michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu inaanza
kutimua vumbi kesho (Agosti 8 mwaka huu) Mjini Kigali.
Azam fc wamechukua nafasi yaYanga sc waliogoma
kuthibitisha kutuma kikosi A kama walivyotakiwa na CECAFA kufikia juzi jioni,
lakini Yanga hawakufanya hilo.
Yanga walitaka kupeleke kikosi cha pili, lakini
CECAFA walisema mashindno ya Kagame siyo ya watoto na hatua ya Yanga ililenga
kuyashushia hadhi, hivyo wakawataka Yanga kupeleka kikosi cha kwanza na
walipogoma waliwasiliana na TFF na kuwataka watume timu nyingine ambapo Azam fc
walipata nafasi hiyo.
Azam fc wanaingia kundi A na kuungana na Wenyeji,
Rayon Sport, Coffee kutoka Ethiopia, Atlabara ya Sudan kusini na KMKM ya
Zanzibar.
Wana Lambalamba watacheza mechi ya kwanza kesho
dhidi ya wenyeji Rayon Sports katika uwanja wa Taifa wa Amahoro jijini Kigali.
Azam wamekubali kwenda kushiriki kwasababu
walihitaji nafasi hiyo na watatuma kikosi kilichotwaa ubingwa msimu uliopita
cha wachezaji 20 pamoja na wachezaji wote wapya iliyowasajili.
Kikosi kilichotumwa Kigali na Azam FC ni: Makipa
Mwadini Ally, Aishi Manula.
Mabeki: Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Waziri
Salum, Abdalallah Kheri, Aggrey Morris, David Mwantika na Said Mourad.
Viungo: Mudathir Yahya, Kipre Balou, Salumu
Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha ‘Vialli’, Farid Musaa na Joseph Peterson.
Washumbuliaji: Didier Kavumbagu, Kipre
Tchetche, Leonel Saint-Preux na John Bocco.
Washambuliaji wawili, Ismail Diara kutoka Mali na
Gaudens Mwaikimba wameachwa katika kikosi hicho.
Benchi la Ufundi litaongozwa na kocha mkuu
Mcameroon, Joseph Marius Omog, kocha msaidizi Kalimangonga Ongala, kocha wa
makipa Idd Abubakar na meneje, Jemadari Said.
0 comments:
Post a Comment