
Na Baraka Mpenja, Dares salaam
Imechapishwa Agosti 7, 2014, saa 12:51 jioni
MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ atatoa burudani ya kufa mtu katika tamasha la ‘Simba
Day’ linalotarajia kufanyika kesho kutwa (Agosti 9, mwaka huu) katika uwanja wa Taifa, uliopo Chang`ombe
jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
amezunguma na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa JB Belmont katikati ya
jiji na kueleza kuwa saabu ya kumchagua Diamond ni kutokana na ukweli kuwa
ndiye msanii anayetamba kwa sasa.
Daimond ambaye kwasasa ‘anasumbua’ na wimbo wa My
Number One na Mdogo mdogo ataungana na bendi ya Twanga Pepeta na wasanii wengine kama vile Dully Sykesm,
Barnaba, Mataalum na makundi ya kudansi kutumbuiza katika tamasha hilo la kila
mwaka.
Mbali na burudani hizo, kutakuwa na mechi mbili za
mpira wa miguuu ambapo timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 20 itachuana na
timu ya vijana ya Azam fc.
Baadaye kikosi kamili cha Simba kitaoneshana kazi
na Zesco United ya Zambia.
Katika mechi hiyo, Simba imeahidi kutumia kikosi
chake kamili ambapo wachezaji wote waliowasajili majira haya ya kiangazi mwaka
huu wataonekana katika mechi hiyo maalum ya kuwatambulisha kwa mashabiki wao.
“Wachezaji wote wataonekana siku hiyo na
mshambuliaji wetu mpya kutoka kenye Kiongera tayari amewasili nchini”. Alisema
Kaburu.
Naye meneja wa Zesco, Mavuto alitamba kuwafunga Simba
katika mechi ya kesho ingawa hana uhakika watawafunga magoli mangapi, lakini
alisisitiza kuwa watafanya vizuri, hivyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa
wingi kesho.
0 comments:
Post a Comment