
Juan Mata (kushoto) alimkaribisha mchezaji mwenzake wa Hispania Ander Herrera (kulia) katika klabu ya Man United.
LICHA ya kucheza pamoja uwanjani, wachezaji wa Manchester United raia wa Hispania wameamua kujenga mahusiano yao nje ya uwanja.
Juan Mata, Ander Herrera na David de Gea wamekuwa marafiki wazuri; walifurahia kula chakula cha mchana pamoja kwenye kijiji cha Hale, mjini Cheshrie jana mchana.
Wachezaji hao watatu wa Hispania wote walicheza katika mechi ya ufunguzi ya ligi kuu England dhidi ya Swansea, lakini walishindwa kuinusuru timu yao na kipigo cha mabao 2-1 katika dimba la Old Trafford.

Wahispania: Kipa wa Manchester United, David de Gea na Herrera walipigwa picha wakitembea pamoja jana.

Nyota hao watatu wakiwa pamoja jana
0 comments:
Post a Comment