
Maoni: Kwa Jose Mourinho ili
aendelee kuwa kocha wa Chelsea kwa msimu ujao na kuendelea basi anahitaji
kushinda aidha ubingwa wa ulaya au Premier League ili kibarua chake kisiote
nyasi. Msimu uliopita alimaliza nafasi ya 3, Roman Abramovich akampa fedha na sasa amenunua wachezaji anaowataka, Felipe
Luis, Diego Costa, Cesc Cesc Fàbregas, na amemrudisha
Didier Drogba kwenye payroll - sasa endapo Mourinho atashindwa kuwapokonya
ubingwa Man City au Real Madrid (ulaya) billionea wa kirusi bila shaka
atamuondoa darajani kwa mara ya pili.

0 comments:
Post a Comment