
Na Baraka Mpenja
AZAM FC wanashuka dimbani leo kukabiliana na El
Merreikh ya Sudan katika mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Afrika
mashariki na kati, Kombe la Kagame inayondelea mjini Kigali Rwanda.
Mechi hiyo kali na ya kukata na shoka itaanza
mapema saa 9:00 alasiri.
Taarifa kutoka Kigali zinaeleza kuwa mechi hiyo
imevuta hisia za mashabiki wengi wa soka kutokana na ubora na viwango vya timu
hizo katika mashindano hayo.
Timu zote mbili zinapewa nafasi ya kutwaa ubingwa,
hivyo mchezo wa leo kuonekana kama fainali iliyokuja mapema.
Meneje wa Azam fc, Jemedari Said amesema wachezaji
wote wameamka salama na wana morali kubwa ya kufanya vizuri ikizingatiwa
walitembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma
Suleiman Nkamia na kumuahidi kupigana kufa na kupona.
Jemedari alisema wachezaji wote wapo salama na
hakuna majeruhi yeyote,nah ii ni nafasi nzuri kwao kocha mkuu, Mcameroon, Joseph
Marius Omog kuamua nani aanze.
“Kila kitu kipo sawasawa na katika mazoezi ya
mwisho jana wachezaji wote walifanya walikuwepo,” alisema Jemedari. “Kwetu ni
kama fainali iliyotujia mapema kwasababu ya namna El Merreikh wanavyocheza
kiufundi na kimbinu.”
“Unapozungumzia El Merreikh, unazungumzia moja
kati ya timu nane bora barani Afrika na wamekuwa wakicheza mara kwa mara hatua
ya makundu ya ligi ya mabingwa, kwahiyo unapoitaja timu hiyo unataja timu
kubwa.”
Mechi nyingine ya Robo fainali itawakutanisha KCC
ya Uganda dhidi ya Altabara ya kusini.
Polisi ya Rwanda ilifanikiwa kufuzu hatua ya nusu
fainali jana baada ya kuifunga kwa penalti 9-8 Atletico ya Burundi.
Hii ilitokana na timu hizo kumaliza dakika 90 kwa
suluhu pacha ya bila kufungana. Hivyo Polisi na APR watakutana nusu fainali.
Nao maafande wa APR waliwatoa Rayon Sport kwa penalti
4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 2-2.
0 comments:
Post a Comment