
Bingwa: Jamie Moore baada ya kuibuka bingwa wa pambano la mashindano ya Jumuiya ya Madola, uzito wa kati dhidi ya Adam Katumwa, katika uwanja wa MEN Arena, Manchester. Aprili 10, 2004.
Imechapishwa Agosti 5, 2014, saa 1:32 asubuhi
HABARI mbaya kwa wapenzi wa masumbwi. Bingwa wa zamani wa ngumi wa Uingereza Jamie Moore amepigwa risasi mara mbili katika mguu wake mjini Marbella.
Bondia huyo mwenye miaka 35 alikuwa katika mji huo wa Hispania akifanya mazoezi kujiandaa na pambano lake la uzito wa kati dhidi Matthew Macklin likalopigwa Dublin mapema mwezi huu.
Moore ameripotiwa kupigwa risasi mara tano mapema jumapili asubuhi na kwasasa yupo hospitalini chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Moore alikutana na Sir Alex Ferguson na Wayne Rooney mwaka 2007


Chanzo kililiambia Manchester Evening News: 'Wakati anapigwa risasi alikuwa ametoka kujivinjari na sio kwenye Gym"
Moore alishinda ubingwa wa uzito wa kati mwaka 2003 na baadaye alitetea dhidi Macklin katika pambano kali la Manchester.
Pia aliibuka bingwa wa Ulaya mwaka 2009, lakini alistaafu baadaye kufuatia kuumwa na ikashauriwa ajikite katika matibabu.
Moore alikosa ubingwa wa dunia na maisha yake ya masumbwi yaliishia kwa kupigwa mara mbili na
Ryan Rhodes na Sergey Khomitsky.
0 comments:
Post a Comment