Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 5, 2014, saa 5:00 asubuhi
BARAZA la vyama vya mpira wa miguu Afrika
Mashariki na kati, CECAFA limeiengua rasmi klabu Yanga kushiri kombe la Kagame
2014 na nafasi yake imechukuliwa na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Azam fc.
Tangu awali, CECAFA walitoa taarifa kuwa Azam
watapewa nafasi ya upendeleo katika michuano hiyo inayoanza kushika kasi Agosti
8 mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda, lakini mpaka jana wana Lambalamba
walikuwa hawana taarifa rasmi.
Yanga sc ndio walitakiwa kushiriki michuano hiyo,
lakini waliamua kupeleka kikosi B ambapo CECAFA ilikikataa na kuitaka timu hiyo
ya makutano ya Twiga na Jangwani, Kariokoo jijini Dar es salaam ipeleke kikosi cha
kwanza pamoja na kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo.
Mpaka jana usiku, Yanga walikuwa hawajathibitisha
kukubaliana na agizo hilo la CECAFA na taarifa zilizoripotiwa na mtandao huu
usiku wa jana ni kwamba Yanga wamegoma kubadili kikosi chao, hivyo
hawatashiriki.
Baada ya Yanga kushindwa kutii Agizo la CECAFA,
viongozi wa baraza hilo wakatuma taarifa TFF wakiagiza timu nyingine iliyo
tayari ipeleke kikosi na ndipo Azam
waliosemwa tangu mwanzo kuwa watashiriki kupata nafasi hiyo.
Azam wamekubali kwenda kushiriki kwasababu walihitaji
nafasi hiyo na watatuma kikosi kilichotwaa ubingwa msimu uliopita cha wachezaji
20 pamoja na wachezaji wote wapya iliyowasajili.
Kikosi kilichotumwa Kigali na Azam FC ni: Makipa
Mwadini Ally, Aishi Manula.
Mabeki: Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Waziri
Salum, Abdalallah Kheri, Aggrey Morris, David Mwantika na Said Mourad.
Viungo: Mudathir Yahya, Kipre Balou, Salumu
Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha ‘Vialli’, Farid Musaa na Joseph Peterson.
Washumbuliaji: Didier Kavumbagu, Kipre
Tchetche, Leonel Saint-Preux na John
Bocco.
Washambuliaji wawili, Ismail Diara kutoka Mali na
Gaudens Mwaikimba wameachwa katika kikosi hicho.
Benchi la Ufundi litaongozwa na kocha mkuu Mcameroon,
Joseph Marius Omog, kocha msaidizi Kalimangonga Ongala, kocha wa makipa Idd Abubakar
na meneje, Jemadari Said.
Azam fc wanaingia kundi A na kuungana na Wenyeji, Rayon
Sport, Coffee kutoka Ethiopia, Atlabara ya Sudan kusini na KMKM ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment