
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 5:40 asubuhi
BOSI wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini
Manchester City itakuwa imelamba dume kama itamsajili kiungo mkongwe Frank
Lampard ambaye yuko mbioni kujiunga Etihad kwa mkopo.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 aliachwa na Chelsea
majira haya ya kiangazi mwaka huu baada ya mkataba wake kumalizika na alisaini
mkataba wa miaka miwili na New York City FC mwezi juni mwaka huu.
Manchester City na New York Yankees wote wana hisa
za umiliki wa New York.
Msimu wa ligi wa Marekani unatarajiwa kuanza mwezi
machi 2015, hivyo Lampard anatakiwa kujiunga na kikosi cha Manuel Pellegrini
kwa mkataba mfupi wa mkopo ili kulinda kiwango chake.
Ancelotti aliyemshuhudia Lampard akiwa mfungaji wa
juu zaidi wakati yupo Stamford Bridge, anaamini nyota huyo wa kimataifa wa
Uingereza atakuwa msaada kwa Man City na akatania kuwa anaweza kumsajili Real
Madrid.
“Sikujua hili. Nimeshangaa sana kwasababu nilijua
anakuja kucheza Marekani,” Alisema Ancelotti ambaye yupo Michigan kukabiliana
na Manchester United.
“Nimechelewe sana, ningemsajili Real Madrid,
lakini nimfurahia sana Frank kwasababu nina kumbukumbu nzuri juu yake. Namtakia
kila la kheri. Ni usajili mzuri kwa Manchester City”.
Lampard alicheza miaka miwili chini ya Ancelotti
na kuiona Chelsea ikishinda kombe la ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Hisani
kabla ya kutimuliwa baada ya kumaliza msimu wa 2011 bila kikombe.
0 comments:
Post a Comment