Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akimkabidhi hundi kiongozi wa Morogoro Youth Football Academy
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 5:22 asubuhi
SHOMARY Kapombe alishakamilisha usajili wake wa kujiunga na
mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc na ataitumikia klabu hiyo
msimu ujao wa ligi kuu na ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kapombe alisajiliwa na Azam kutoka klabu ya AS Cannes ya
Ufaransa ambapo aliuzwa na Simba chini ya uongozi wa Ismail Aden Rage.
Katika mauzo ya kapombe, kulikuwa na kipengele cha Simba kupata
asilimia kadhaa kama mchezaji huyo atauzwa klabu yoyote duniani.
Baada ya Kapombe kuuzwa Azam, Simba walitakiwa kulipwa milioni
60 kama mkataba unavyoelekeza.
Kulikuwa na mvutano wa kulipwa fedha hizo, lakini Azam wameamua
kumalizana na Simba ambapo jana waliipa klabu hiyo ya Msimbazi milioni 60 baada
ya kumnunua Kapombe.
Lingine kubwa zaidi, jana simba imewakabidhi ‘Morogoro youth
Football academy’ milioni 9 kama share ya kituo kwa mauzo ya Mchezaji shomari
Kapombe.
Wakati simba inamsajili Kapombe kutoka kwenye kituo kulikuwa na
makubaliano ya kuwapa 15% on ward sale.
Hiki ni kitendo cha kuigwa na klabu nyingine zenye utaratibu wa
kuchukua wachezaji vijana
0 comments:
Post a Comment