
Na Baraka Mbolembole
Imechapishwa Julai 9, 2014, saa 11:04 usiku
Mshambulizi wa Kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samata ameuambia mtandao huu kuwa atatua nchini, tarehe 16 ili
kuongeza nguvu katika kikosi cha Taifa Stars.
Samata ambaye alikuwa na
majeraha ambayo yalimfanya aukose mchezo wa marejeano kati ya Tanzania na
Zimbamwe, Mwezi uliopita, kwa sasa yupo fiti
japo hajacheza mchezo wowote tangu alipotoka katika maumivu.
" Nitakuja kambini tarehe 16 inshallah
panapo majaAliwa, naendelea vizuri kwa sasa japokuwa sijacheza mchezo wowote
tangu nilipotoka katika maumivu" anasema mshambulizi huyo wakati alipokuwa
akiwasiliana na mwandishi wa mtandao huu.

Samatta, mchezaji wa klabu bingwa mara nne ya
Afrika, TP Mazembe ya DRC, amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu sana katika timu
ya Taifa ya Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu sasa na atatua nchini ili
kuungana na kikosi hicho cha kocha Martin Nooij katika kambi ya Tukuyu, Mbeya.
Hiyo itakuwa ni muendelezo wa
kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi kuwania tiketi ya
kucheza michuano Afrika Mwakani nchini Morocco.
Stars itacheza na timu ya Taifa
ya Msumbiji, mwishoni mwa wiki ijayo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano
na kitendo cha nyota huyo kuwasili nchini kitamaliza hofu ya Watanzania ambao
wamekuwa na wasiwasi na upatikanaji wa mchezaji huyo katika timu ya Taifa
kutokana na mara kwa mara kuzuiwa na klabu yake.
Wakati huohuo mshambulizio huyo amesema kuwa
timu ya Taifa ya Brazil imepata aibu kubwa baada ya kukubali kipigo cha mabao
7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia usiku
wa kuamikia leo. Brazil ilifungwa mabao hayo ikiwa mwenyeji na kitendo hicho
kimemfanya, Samata kusema: " Hakika Brazil wamepata aibu kubwa sana, ila
ndio mpira ulivyo' alisema kwa ufupi mshambulizi huyo.
Chanzo:shaffihdauda.com

0 comments:
Post a Comment