
Imechapishwa Julai 9, 2014, saa 11:25 jioni
UJERUMANI IMEPAA JUU ZAIDI
• Kwa kufunga bao la pili,
Miroslav Klose amekuwa mfalme wa kufunga mabao katika fainali za kombe la
dunia. Klose kwasasa amefikisha mabao 16 katika maisha yake ya soka na kuvunja
rekodi ya Gwiji wa Brazil, Ronaldo.
• Ujerumani
walifunga mabao 5 katika dakika 29 za kwanza, nchi hii imekuwa ya kwanza
kufunga kwa haraka mabao matano katika muda wa mechi. Rekodi ilikuwa inashikiliwa
na Yugoslavia ambao walifunga mabao matano katika dakika 30 dhidi ya Zaire
mwaka 1974.
• Magoli 7 ya Ujerumani yamevunja
rekodi ya mabao mengi zaidi kufungwa katika fainali za kombe la dunia, mwanzoni
ilikuwa sita kati ya Uruguay na Argentina mwaka 1930, na Ujerumani Magharibi
mwaka 1994. Hakuna aliyewahi kufunga hata mabao matano katika hatua ya nusu
fainali tangu Brazil waifunge Ufaransa mabao 5-2 mwaka 1958.

• Bao la sita lilivunja rekodi
ya mabao matano ya nusu fainali ya kombe la dunia.
• Ujerumani sasa imekuwa
nchi iliyofunga mabao mengi kwa wakati wote wa historia ya kombe la dunia.
Imefunga magoli 223. Waliipita Brazil yenye mabao 220 katika kipindi cha kwanza
kwenye mechi ya jana.
• Ujerumani wameweza
kuongoza mara tatu kwa mabao matano katika fainali za kombe la dunia- walifanya
hivyo dhidi ya Saudi Arabia (2002) ambapo walishinda 8-0, walifanya hivyo dhidi
ya Mexico mwaka 1978 waliposhinda mabao 6-0 na walifanya hivyo dhidi ya Uswisi
mwaka 1966 waliposhinda 5-0.

•Ujerumani
imefika fainali za kombe la dunia mara nyingi zaidi kuliko taifa lolote.
Imefika fainali mara nane mpaka sasa.
• Thomas Muller anakuwa mchezaji wa 13 kufunga mabao 10 katika fainali za
kombe la dunia na anakuwa mchezaji wa pili kufunga magoli matano mfululizo
katika fainali za kombe la dunia baada ya Klose mwaka 2002 na 2006.
IMEISHUSHA HADHI BRAZIl
• Kipigo
cha Brazil kimevunja rekodi yao waliyoweka mwaka 1920 walipofungwa mabao 6-0
dhidi ya Uruguay katika mchezo ya Copa Amerika.

• Brazil hawajawahi
kufungwa mabao matano katika fainali za kombe la dunia tangu mwaka 1998.
Waliruhusu mabao manne katika mechi tano mwaka 2010, mabao mawili katika mechi
tano mwaka 2006 na mabao manne katika mechi saba za mwaka 2002.
• Brazil haijawahi kufungwa mabao manne katika mechi
yoyote ya kombe la dunia. Katika mechi zake 102 ilizocheza kabla ya jana.
• Brazil wameruhusu mabao
matano mara nane kwenye michezo maalumu—sita mwaka 1960 au kabla na mara mbili
mwaka 1963. Magoli sita? Sio, tangu
mwaka 1940. Saba? Sio, tangu
walipofungwa mabao 8-4 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Yugoslavia mwaka 1934.

• Rekodi mbaya ya nchi
mwenyeji kufungwa mabao mengi ilikuwa mwaka 2010 ambapo Afrika kusini ilipoteza
kwa mabao 3-0 dhidi ya Urugauy. Mexico ilifungwa mabao 4-1 na Italia mwaka 1970
na Sweden ilifungwa mabao 5-2 na Brazil mwaka 1958.
•
Brazil imepoteza kwa mara ya kwanza mechi za mashindano ilizocheza nyumbani tangu
mwaka 1975 walipofungwa na Peru kwenye michuano ya Copa Amerika—imepita miaka
63.
• Kwa
mara ya mwisho Brazil kupoteza mechi ya kombe la dunia nyumbani ilikuwa mwaka
1950 na kusababisha timu kubadili jezi zake.

0 comments:
Post a Comment