Wednesday, July 9, 2014

Running riot: Germany scored four goals in six first-half minutes during Tuesday's semi-final against Brazil
Ujerumani wameipiga Brazil kipigo cha mbwa mwizi.

Na Baraka Mpenja

KWA Muda mrefu wananchi wa Brazil waliandamana wakipinga nchi yao kuandaa fainali za kombe la dunia kwasababu kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa.
Walikuwa wakihuzunishwa na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuandaa miundo mbinu ya kombe la dunia, wakati maisha yao yakiwa katika hali mbaya.
Huduma mbovu za jamii, umasikini wao uliwahamasisha kuandamana na kuleta sintofahamu ya kisiasa.

Brazil walienda kwa kujivuta na mnamo juni 12 mwaka huu wakasahau shida zote na kushuhudia timu yao ya Taifa ikicheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia.
Walipata ushindi wa mabao 3-1 na kufurahia matokeo hayo.
Faraja pekee kwa wananchi maskini wa Brazil ilikuwa ni kuona timu yao inafanya vizuri na kubeba kombe. Walikuwa wanafurika uwanjani, kwenye kumbi za kuoneshea mpira, lengo ni kutaka kuona timu yao inafanya nini.
Disbelief: Fernandinho, Maicon and David Luiz look bemused following Germany's fifth goal of the evening
Hawaamini: Fernandinho, Maicon na David Luiz 

wakishangaa baada ya Ujerumani kufunga bao la tano.
Brazil ambayo unaweza kusema ni mbovu kuliko Brazil zote zilizopita, ilijikongoja hatua ya makundi na kuingia hatua ya 16.
Baada ya hapo walipigiwa mbungi kubwa na Colombia, lakini walifanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali.
Kwa bahati mbaya wakiwa na ubovu wao, waliingia mikononi mwa `watu katili`, Ujerumani.
Kabla ya mechi, kocha Luiz Felipe Scorali alijigamba kuifunga Ujerumani na katika mkutano wa jana na waandishi wa habari alithubutu kuuzungumzia mchezo wa fainali, tena dhidi ya Argentina.
Kwa bahati mbaya hakufirikiria kama anaenda kukutana na Ujerumani yenye bunduki zote.
Opener: Thomas Muller scores Germany's first to set Joachim Low's men on their way
 Thomas Muller akiifungia Ujerumani bao la kuongoza 
Back of the net! Goalkeeper Julio Cesar is powerless to stop Thomas Muller's effort as David Luiz watches on
Mlinda mlango, Julio Cesar hakuwa na ujanja wa kuzuia mpira uliopigwa na Muller, huku David Luiz akishangaa .

Brazil ambayo unaweza kusema ni mbovu kuliko Brazil zote zilizopita, ilijikongoja hatua ya makundi na kuingia hatua ya 16.

Baada ya hapo walipigiwa mbungi kubwa na Colombia, lakini walifanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali.
Kwa bahati mbaya wakiwa na ubovu wao, waliingia mikononi mwa `watu katili`, Ujerumani.
Kabla ya mechi, kocha Luiz Felipe Scorali alijigamba kuifunga Ujerumani na katika mkutano wa jana na waandishi wa habari alithubutu kuuzungumzia mchezo wa fainali, tena dhidi ya Argentina.
Kwa bahati mbaya hakufirikiria kama anaenda kukutana na Ujerumani yenye bunduki zote.
Saa hazigandi, majira ya saa 5 usiku, ngoma ikaanza katika dimba la Estaduuio Mineirao, huku Neymar na Thiago Silva wakikosekana.
Kama masihara vile, Ujerumani walianza kuchezea nyavu za Brazil mapema.
Historic: The strike that made hm the record holder
Watu wakajua kawaida, lakini mvua iliyokuja kwa Wabrazil ikuwa kubwa mno.
Beki mbovu ya Brazil ilipitisha mipira mingi. Dante, Luiz, Marcelo, Maicon, daaah! siku ilikuwa mbaya kwao.
Watu wote waliovaa nguo za njano walitamani mpira uishe.
Brazil usiku huu imefungwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa fainali ya kwanza ya kombe la dunia.
Hii ni rekodi mbaya katika soka la Dunia. Brazil inakuwa nchi ya kwanza kufungwa mabao mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia tangu lianze mwaka 1930 nchini Uruguay.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na  Muller, 11, Klose, 23, Kroos, 24, 26, Khedira, 29, Schurrle, 69, 79.
Bao pekee la Brazil limefungwa na Oscar katika dakika za lala salama.

0 comments:

https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video