
Imechapishwa Julai 4, 2014, saa 4:15 asubuhi
RON Vlaar amepotezea usemi kuwa mechi ya kesho jumamosi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Costa Rica haitakuwa mechi rahisi kwa Uholanzi.
RON Vlaar amepotezea usemi kuwa mechi ya kesho jumamosi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Costa Rica haitakuwa mechi rahisi kwa Uholanzi.
Wakiwa wameshinda kila mechi
waliyocheza Brazil, Uholanzi ndio wanapewa nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali
dhidi ya timu iliyofika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, Vlaar anawahofia Cota Rica
kwa kiwango walichoonesha mechi za nyuma dhidi ya mabingwa wa zamani wa dunia,
Italia, Uruguay na England kabla ya kuwatandika mabingwa wa Euro 2014, timu ya
Taifa ya Ugiriki katika hatua ya pili.
“Mechi hizi hazishindiki kirahisi,”
beki wa Aton Villa aliuambia mtandao rasmi wa klabu. “Hakuna mechi rahisi”.
“Costa Rica waliwafunga Uruguay na
Italia na walitoka sare na England. Waliwafunga Ugiriki”.
“Itakuwa mechi ngumu tena-lakini
tunatazama mbele. Ni changamoto kubwa tena”.
Vlaar alisema, Uholanzi iliyoifunga
Hispania mabao 5-1 kwenye mchezo wa ufunguzi,
ina imani kubwa ya kufanya vizuri dhidi ya Costa Rica, mjini Salvador.
“Tuna morali kubwa kambini,” beki huyo
wa kati aliongeza. “Tumefanya vizuri sana. Tumeshinda mechi zote, ni vizuri”.

0 comments:
Post a Comment