Friday, July 4, 2014

Brazil will be at their peak - Pekerman
Imechapishwa Julai 4, 2014, saa 3:47 asubuhi

KOCHA wa Colombia, Jose Pekerman anatarajia kuwaona Brazil wakiwa katika kiwango chao bora kuelekea  katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia utakaopigwa kuanzia majira ya saa 5 usiku wa leo.

The Selecao wamekuwa wakikosolewa na vyombo vya habari vya nchini mwao kwa kiwango chao `mbofu mbofu` katika mashindano ya mwaka huu, hususani baada ya kupata ushindi wa kubahatisha wa mikwaju ya penati dhidi ya Chile hatua ya 16.

Pekerman hatarajia kuwaona wenyeji wakiwa na presha baada ya mchezo wa Fortaleza  dhidi ya Chile.

“Kufuzu nusu fainali ni matarajio makubwa na kila timu itacheza kwa kiwango chake cha juu ili kupata  nafasi hiyo”.

“Kwa timu zote mbili tunaweza kuona wachezaji wakubwa, na wachezaji wakubwa wanapokuwepo timu zote, mechi inakuwa na mvuto mkubwa”.

Inajadiliwa nchini Brazil kuwa matumaini makubwa ya wenyeji kufuzu, yanaweza kuwapa nafasi Colombia kufuzu pia, japokuwa Pekerman hawezi kuyaamini maneno hayo.


“Timu yetu mara zote inaangalia mbele,” alieleza. “Kwa Colombia, kila mechi ni changamoto mpya. Kwahiyo hatuwezi kutazama nyuma kwa kile tulichofanya. Jambo la msingi ni kutojihisi kama tuna nafasi. Tutauchukuliwa mchezo huu kama tulivyocheza mechi za nyuma”.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video