Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MICHAEL Richard Wambura ameibuka tena na
kumshangaa Rais mpya wa Simba, Evans
Elieza Aveva na kamati yake ya utendaji kwa kufanya maamuzi ya kulipeleka suala
lake kwenye mkutano mkuu wa agosti 3 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam, Wambura amesema hakuna haja ya kupeleka suala lake kwenye mkutano
huo kwasababu sakata lake lilimalizwa na kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF
chini ya mwenyekiti wake, Jaji Julius Mutabazi
Lugaziya.
Wambura ameyasema hayo ikiwa ni jana tu, ambapo Aveva alitangaza kuwasimamishwa
wanacha 69 kwa kosa la kwenda mahakama ya kawaida kujaribu kuzuia uchaguzi wa
Simba na alisema suala lao litajadiliwa kwenye mkutano mkuu wa mwezi agosti,
sanjari na suala la Wambura la kuipeleka Simba mahakamani mwaka 2010.
Lakini `Kidume` Wambura amekuja juu na kusema yeye
alishasafishwa na kamati ya Lugaziya na kitendo cha Aveva kuwapiga `Stop` wanachama
ni kuendelea kuchochea migogoro isiyokuwa ya lazima.
“Mimi nilisafishwa kwenye kamati ya Rufani ya Lugaziya na ndio maana nilirudishwa
kwenye mchakato wa uchaguzi, na niliondolewa kwa kosa la kupiga kampeni kabla
ya muda, hivyo sina haja na mkutano huo”. Alisema Wambura.
Wambura aligusia Ibara ya 41(d) ya klabu ya Simba
ambapo alifafanua kuwa kuwanyima wanachama fursa ya kujitetea na kusikilizwa
kabla ya kuchukua hatua ni uvunjifu wa haki za msingi za binadamu.
Aidha, Wambura
alisema wanachama waliokwenda mahakamani wasipuuzwe kwasababu wana hoja za
msingi.
“Wangekuwa hawana hoja, hata mahakama kuu
isingewapa haki ya kufungua shauri lao. Wasipuuzwe, wapewe fursa ya kujitetea
na kusikilizwa”. Aliongeza Wambura.
Alisisitiza kuwa Ibara ya 54(3) ya klabu ya Simba
inafafanua kuwa uamuzi wowote wa kufukuza wanachama lazima upigiwe kura za siri
na wajumbe theluthi mbili waunge mkono, huku akitolea mfano wa Hassani Dalali
alipofanya jaribio la kumpinuda Mwina Kaduguda, lakini alikwama kwasababu
wanachama walikataa pendekezo lake.
Aliongeza kuwa uongozi wa Aveva hauwezi kupambana
na wanachama zaidi ya 500 na kama utaendelea kufanya hivyo basi utaingia katika
mgogoro mkubwa, lakini akashauri uongozi utafute suluhusho la mapema.
Wambura alisema ushauri wake atauwasilisha kwa
maandishi kwa uongozi wa Simba sc kama sehemu kutunza kumbukumbu kuwa
aliyaongea hayo.

0 comments:
Post a Comment