
Afisa habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa na Coutinho (kulia) baada ya kuwasili nchini jana akitokea kwao nchini Brazil
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
Imechapishwa Juni 28, 2014, saa 4:00 asubuhi
YANGA SC imemsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Andrey Marcel Ferreira Coutinho.
YANGA SC imemsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Andrey Marcel Ferreira Coutinho.
Mchezaji
huyo aliwasili jana mchana jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil
tayari kwa kuanza kazi ya kuitumikia Yanga katika msimu wa 2014/2014 wa ligi
kuu soka Tanzania bara.
Coutinho
aliwaeleza waandishi wa habari kuwa anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi
ambayo watu wake wanapenda mpira.
Mchezaji
huyo haijui Tanzania, lakini ameifahamu kutokana na bosi wake Marcio Maximo
ambaye amechangia kwa asilimia zote kumleta nchini.
Bila
shaka wakati wanaongea na Maximo juu ya kuja kufanya kazi Tanzania, Coutinho
alihoji mambo mengi na mazingira ya Tanzania na kupewa majibu na Maximo ambaye
unaweza kusema ni mwenyeji wake.
Maximo
anafahamu utamaduni wa mashabiki wa Tanzania na alimweleza ukweli kiungo huyo na
yeye kuiamini Tanzania mpaka kusema anafurahia kufanya kazi kwenye ardhi ya
nchi hii ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Brazil
kuna wachezaji wengi na vipaji vingi vya soka. Hii ni nchi inayosemekana
kunukia mpira kila kona.
Tunaona
wabrazil wengi wanafanya makubwa katika soka la sasa duniani, lakini miaka ya
nyuma walitokea wachezaji wakali pia.
Unamkumbuka
Pele? Huko mbali, miaka ya karibuni tu, akina Ronaldo, Ronaldinho, Ricardo
Kaka`, Robinho, na sasa Neymar wametikisa soka la dunia.
Hawa
ni mfano tu, ukiamua kuwataja wachezaji wa Brazil waliofanya kazi nzuri
utaandika kwa muda mrefu na huwezi kumaliza, lakini ninachojaribu kusema ni kwamba, Brazil
ni nchi yenye vipaji vingi vya soka.
Kwa
wale waliobahatika kufika Brazil, wanajua wazi kuhusu hilo. Ukipita mitaa mingi
ya nchi hii, lazima uwakute vijana wanacheza soka.
Katika
maelezo ya Coutinho alisema amewahi kucheza barani Asia na alipata uzoefu
mzuri, hivyo anaamini chini ya makocha aliowazoea ataisaidia Yanga.
Kucheza
Asia sio jambo jepesi, huko pia kuna mpira na watu wana mipango mizuri.

Anaujua Mpira?: Coutinho anaanza mazoezi jumatatu chini ya kocha Marcio Maximo.
Watu
wengi wanabeza suala la Yanga kumsajili Coutinho. Maneno ya kejeli yanasikika
hasa kutoka upande wa pili. Utasikia Coutinho sio mchezaji, muuza `madafu` tu
huko Brazil.
Wengine
wanahoji, angekuwa mchezaji mzuri si angecheza huko huko Brazil?, kwanini aje
Yanga, tena Tanzania huku ambako mpira tunautafuta kwa `tochi`.
Kuna
kitu kimoja lazima tukumbushane, katika maisha ya mwanadamu, kuna matabaki
makubwa matatu.
Kuna
tabaka la juu, la kati na la chini, yawezekana likawepo la chini kabisa.
Ukiingia
kiuchumi, tabaka la juu unazungumzia watu wenye mkwanja mrefu, tabaka la chini
ni wale wanaofuatia, la chini ni wale wenzangu na mimi, la chini kabisa, huko
kuna balaa.
Hata
katika mpira, kuna matabaka ya wachezaji, wapo wa kiwango cha juu, hapa unataja
akina Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Luis Suarez, Wayne Rooney, Andrea Pirlo,
Karim Benzema na wengi wengi ambao siwezi kuwataja.
Pia
kuna tabaka la kati, hapa ndio kuna wachezaji wengi, barani Ulaya, Amerika
kusini, Amerika kaskazini, Asia na kwingineko.
Kuna
tabaka la chini. Hapa kuna wachezaji wengi pia kutoka mabara yote.
Lipo
tabaka la chini kabisa, huku sasa kuna wachezaji wengi wanaosaka nafasi za
kusogea mbele. Yawezekana katika viwango vya dunia, Watanzania tukawa kwenye
tabaka hili.
Lakini
kuna tofauti kati ya mchezaji wa tabaka la chini wa Brazil na wa Tanzania.
Tofauti hii inaweza kutokana na kiwango cha taifa katika viwango vya FIFA.
Mchezaji
wa mtaani nchini Brazil, Hispania, Ujerumani anaweza kuwa na kiwango cha juu
zaidi ya Mrisho Ngassa, John Bocco, Ramadhan Singano, hawa ni mfano tu, sina
nia mbaya.
Sisemi
Coutinho anaweza kuwa mkali zaidi ya wachezaji wote wa Tanzania eti tu
kwasababu anatoka Brazil, lakini najaribu kueleza kuwa dharau kabla ya kumuona
mtu akicheza sio jambo la busara.
Yawezekana
yakawa ni maneno ya watani wa jadi kwasababu yamezoeleka, lakini dhana ya
kumdharau mchezaji kabla ya kumuona lazima izungumzwe.
Binafsi
sijawahi kumfuatilia mchezaji huyu kwa undani, ingawa nina habari zake kidogo.
Lakini hainipi sababu ya kusema atawafaa Yanga au hapana.
Kinachotakiwa
ni kusubiri kumuona anafanya mazoezi chini ya Maximo, na uwezo wake utaonekana
hadharani.
Mpira
wa miguu ni mchezo wa hadharani, kama Coutinho ni mkali, wote tutamuona kuanzia
jumatatu.
Lakini
tahadhari lazima iwepo, kumuona kwenye mazoezi kwa siku mbili tatu sio sababu
ya kusema hafai au anafaa. Mpira una mambo mengi, leo hii anaweza kuchemsha,
lakini kesho akafanya vizuri.
Suala
la kumpa muda ni muhimu. Lazima aangaliwe zaidi. Siamini kama Maximo kambeba
bila kumjua. Yeye ni kocha na kufundisha mpira ni kazi yake, hawezi kuleta mtu
atakayemharibia kazi.
Coutinho
kwa bahati nzuri amegundua kuwa atakabiliana na changamoto zikiwemo za
kimazingira. Lakini Maximo lazima amemwambia tabia ya mashabiki wa Kibongo.
Unaweza
kufanya kazi nzuri, lakini ukaharibu kwenye mechi ya watani wa jadi, ukaambulia
kusasambuliwa na kutukanwa.

Big Bosi! Marcio Maximo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam
Sio
wakati muafaka wa kumuita Coutinho muuza `madafu` Brazil, lazima aheshimike na
tusubiri kuona vitu vyake.
Hawezi
kuwa kama Oscar, Neymar, Willian, Fred. Nilisema kuna matabaka katika maisha ya
soka. Hata kama ni wa kiwango cha chini, lazima ukumbuke wewe uko tabaka gani.
Unajua
Yanga kwanini haiwezi kumsajili Neymar au Oscar? Kwasababu ipo tabaka la chini
kulinganisha na Barcelona na Chelsea.
Mbuzi
hula kutokana na urefu wa kamba yake, Yanga wanamuweza Coutinho, waacha
wamtumie. Wenyewe wakiona anafaa wataendelea naye, wakiona `Galasa` watatangaza
kumuacha. Mpira sio vita.
Cha
msingi tusubiri kuona Coutinho ana nini, baada ya hapo tutapata cha kuandika na
kuzungumza.
Sina
maslahi na Yanga wala Coutinho, nina maslahi na soka la Tanzania. Sipendi
kuzungumza kitu ambacho sijakiona. Huwezi kutabiri mchezaji Fulani muuza `madafu`
au mkali wakati kichwani mwako huna hata kumbukumbu ya kumuona akicheza.
“Coutinho
welcome in Tanzania” ukutane na mashabiki wa Kibongo ulioambiwa wanapenda
mpira. Kweli wanapenda, lakini suala la uvumilivu kidogo limewapiga chenga ya
mwili.
0 comments:
Post a Comment