
Licha ya kupoteza nafasi nyingi, Torres alifunga bao moja

Imechapishwa Mei 31, 2014, saa 1:30 asubuhi
NYOTA wa Chelsea, Fernando Torres aliifungia Hispania bao muhimu katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bolivia.
Mechi hiyo ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya kombe la dunia ilipigwa jana usiku na Torres angefunga zaidi ya bao moja, lakini kukosa umakini kulimgharimu.
Toress alifunga bao hilo katika dakika ya 51 kwa njia ya mkwaju wa penati na katika dakika ya 84, Andres Iniesta aliifungia Hispania bao la pili.
Hispania wanakwenda Brazil kutetea ubingwa wao waliotwaa mwaka 2010 nchini Afrika kusini kwa kuwafunga Uholanzi bao 1-0 katika mechi ya fainali.
Kikosi cha Bolivia:
Quinonez, Bejarano, Raldes (Zenteno, 90), Melean (Miranda, 64), Eguino.
Gutierrez, Chumacero (Da. Bejerano, 64), Di. Bejarano, Mojica (Cardozo,
72), Arce (Arze, 72), Moreno (Pena, 82).
0 comments:
Post a Comment