![]() |
| Kaburu |
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 9:30 leo asubuhi.
Dar es Salaam. Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na wagombea wa ujumbe wa kamati ya utendaji ya Simba wamewekewa pingamizi la kuwania uongozi.
Dar es Salaam. Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na wagombea wa ujumbe wa kamati ya utendaji ya Simba wamewekewa pingamizi la kuwania uongozi.
Mwanachama Swaleh Madjapa kadi namba 00574, Mwinyi
Dossy kadi namba 564 pamoja na kocha wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ ndio waliojitokeza jana kuweka pingamizi kwa wagombea hao.
Mbali na Wambura na Kaburu, wajumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Simba, Swedi Nkwabi, Said Pamba, Ibrahimu ‘Maestro’,
Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Daniel Manembe wamewekewa pingamizi na wanachama
watatu tofauti kwa madai ya kukiuka katiba ya Simba.
Madjapa alimwekea pingamizi Wambura akidai
wakati akichukua fomu alifanya kampeni kinyume na taratibu na kwamba ana vielelezo
vyote vinavyothibitisha kuwa Wambura alifanya kampeni kabla ya muda wake.
Wambura aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo,
lakini akasimamishwa na uongozi baada ya kufungua kesi mahakamani kupinga
kuenguliwa kwenye uchaguzi mwaka 2008, kitendo ambacho ni uvunjaji wa katiba.
Pia aliwawekea pingamizi wagombea wote ambao ni
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba inayomaliza muda wake kwa kile
alichoeleza kuwa kwa kipindi cha miaka minne walichokaa madarakani hakuna
walichofanya cha maana kinachofanya waombe tena kupewa miaka mingine minne ili
wamalizie, zaidi ya vurugu.
![]() |
| Wambura |
Naye Kihwelo, anayegombea nafasi ya makamu wa
rais, aliwekea pingamizi Kamati ya Utendaji kwa kile alichodai walikiuka katiba
kwa kuendesha vikao visivyo halali na kuupindua uongozi wa Ismail Aden
Rage na pia walikiuka katiba ya klabu hiyo kwa kutojaza nafasi ya makamu
mwenyekiti iliyoachwa na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ndani ya siku 90.
Pia, wajumbe hao wa kamati ya utendaji inayomaliza
muda wake waliwekewa pingamizi na Mwinyi Dossy kadi namba 564.
Kaburu aliwekewa pingamizi na mchezaji wa zamani
wa klabu hiyo, Athurh Mwambeta (kadi namba 01005) ambaye pia amewekewa na Swedi
Nkwabi. Mwambeta amedai Kaburu akiwa makamu mwenyekiti alikiuka katiba ya Simba
ibara ya 33 (5) na 28 (1b) kwa kushindwa kuwasilisha ripoti ya mapato na
matumizi ya fedha katika mkutano mkuu mwaka 2010 hadi mwaka 2013 alipojiuzulu.
Pia, alidai kuwa kwa mujibu wa katiba ya Simba
kiongozi anayejiuzulu haruhusiwi kugombea tena uongozi ndani ya klabu hiyo kwa
vipindi vitatu na kudai kuwa Kaburu hajafikisha vipindi vitatu toka ajiuzulu.
Kwa upande wa pingamizi la Nkwabi, Mwambeta alidai
kuwa alikiuka katiba wakati wa uongozi wao kwa kuendesha mapinduzi ya kumpindua
Rage. Swedi pia aliwekewa pingamizi na Lucas Mbapila kwa madai ya kukiuka
kanuni za uchaguzi.
Chano Almas aliwekewa pingamizi Dossy na Madjapa
kwa madai ya kukiuka katiba.
wakati akiwa mweka hazina wa klabu hiyo.
Chanzo: Mwananchi



0 comments:
Post a Comment