![]() |
| Victoria University wanaanza kampeni yao leo |
Imechapishwa mei 23, 2014, saa 10:00 leo asubuhi
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MICHUANO mipya ya CECAFA Nile Basin Cup inatarajia
kuanza kutimua vumbi nchini Sudan leo ijumaa kwa mechi tatu kupigwa kwenye
viwanja viwili tofauti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na CECAFA kwa MPENJA BLOG asubuhi hii, Victoria
University kutoka nchini Uganda atakabiliana na Malakia FC kutoka Sudan Kusini
katika uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum majira ya saa 11:30 jioni.
Baadaye katika uwanja huo huo, wenyeji, Al-Merreik
wataoneshana kazi na timu ya Polisi kutoka visiwani Zanzibar majira ya saa 2:00
usiku.
Mbali na mechi hizo za Khartoum, mechi nyingine
itapigwa mjini Shandi, ambapo wenyeji Al-Shandi watavaana na wageni, Dkhill FC kutoka
nchini Djibouti.
Kueleka katika mechi za leo, makamu wa rais wa CECAFA,
Lawrence Mulindwa amezitaka timu zote kucheza mpira kwa kiwango cha juu na
kuzingatia nidhamu wakati wote wa mashindano.
Aidha, Mulindwa ameishukuru serikali ya Sudan kwa kukubali
kudhamini michuano hii mipya.
“Sisi kama CECAFA tunaishukuru sana serikali ya Sudan
kukubali kudhamini mashindano haya. Tunaomba vyombo vya habari vitoe sapoti kwa
mashindano haya”. Alisema Mulindwa katika mkutano na waandishi wa habari jana
jioni katika Hoteli ya Grand Holiday Villa.
Akizungumza katika mkutano huo huo, katibu mkuu wa
CECAFA, Nicholas Musonye alikanusha taarifa zilizoenea kuwa mashindano hayo yapo
kwa ajili ya mambo ya siasa.
“Mashindano haya hayahusiana na siasa hata kidogo. Mto
Nile unashikilia maisha ya mamilioni ya watu (hususani hapa Sudan na Misri) na
sisi kama wadau wa soka tunatakiwa kuhakikisha maji yanatunza maisha ya watu
bila matatizo”. Alisema Musonye wakati akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa
habari.
Kuhusu klabu mbili za Misri zilizojitoa katika
mashindano hayo, Musonye alisema timu hizo mbili zilitaka mashindano yasogezwe
mpaka mwezi julai, jambo ambalo haliwezekani.
Wakati huo huo CECAFA wamesema Mbeya City wanawasili
leo ijumaa nchini Sudan na wanatarajia kutua Khatoum mchana wa leo.
Mbeya city fc wataanza kampeni zake kesho majira ya
11:30 jioni, mjini Khartoum dhidi ya AcademieTchite ya Burundi.
Nao AFC Leopards kutoka Kenya watasili kesho jumamosi
kwa ndege ya shirika la Rwanda.


0 comments:
Post a Comment