
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 9:47 Alasiri
Taifa Stars na Malawi (Flames) zinapambana kesho (Mei 27 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni.
Malawi tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mechi hiyo wakati Taifa Stars iliyopiga kambi yake Tukuyu mkoani Mbeya
inawasili jijini Dar es Salaam kesho (Mei 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ndege
ya Air Tanzania.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 kwa
viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio
kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Hiyo itakuwa ni mechi ya mwisho ya majaribio kwa Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kabla ya kwenda jijini Harare
kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty
Warriors).
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani
Young Chidmozi nayo itakuwa inacheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla ya
kwenda N’djamena kuikabili Chad.
0 comments:
Post a Comment