
Nyota huyo wa klabu ya Monaco alikuwa katika hatihati ya kushiriki kombe la dunia kutokana na kuumia vibaya goti lake kwenye mchezo wa Coupe de France mwezi junuary mwaka huu.
Hata hivyo mwezi uliopita nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid alisema anahitaji mwezi mmoja kuimarika zaidi, lakini Pekerman ameamua kumujumuisha mshambuliaji huyo hatari.
Falcao alifunga mabao 9 katika mechi 13 za kuwania kufuzu kombe la dunia na alishirikiana vizuri sana na wachezaji,
Jackson Martinez na mchezaji wa Borussia Dortmund, Adrian Ramos.
Colombia wataanza kampeni zao za kombe la dunia katika kundi C dhidi ya Ugiriki Juni 14.
Kikosi kizima:
Walinda mango: Faryd Mondragon (Deportivo Cali), David Ospina (Nice), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe)
Walinzi: Santiago Arias (PSV), Pablo Armero (Napoli), Eder Alvarez Balanta (River Plate), Aquivaldo Mosquera (America), Luis Perea (Cruz Azul), Carlos Valdes (San Lorenzo), Mario Yepes (Atalanta), Cristian Zapata (Milan), Camilo Zuniga (Napoli)
Viungo: Abel Aguilar (Toulouse), Juan Cuadrado (Fiorentina), Fredy Guarin (Inter), Victor Ibarbo (Cagliari), Alex Mejia (Atletico Nacional), Juan Fernando Quintero (Porto), Aldo Ramirez (Morelia), James Rodriguez (Monaco), Carlos Sanchez Moreno (Elche), Elkin Soto (Mainz), Macnelly Torres (Al Shabab), Edwin Valencia (Fluminense)
Washambuliaji: Carlos Bacca (Sevilla), Radamel Falcao (Monaco), Teofilo Gutierrez (River), Jackson Martinez (Porto), Luis Muriel (Udinese), Adrian Ramos (Hertha Berlin)
0 comments:
Post a Comment